Monday, April 12Kiswahili kitukuzwe!

Tag: Ushairi

Nadharia ya Uhakiki wa Ushairi
Nukuu Kidato cha nne

Nadharia ya Uhakiki wa Ushairi

Uandishi wa ushairi Picha na Pixabay Ili kuhakiki ushairi tunatumia vipengele vya fani na maudhui kama ilivyo katika kazi zingine za kisanaa. MAUDHUI Hapa tunachunguza vipengele kama vile; dhamira, ujumbe, falsafa, mtazamo na migogoro. Vipengele hivi vinasaidia kuelimisha jamii. FANI Tunajikita katika kuchunguza; Mtindo, muundo, wahusika, mandhari na matumizi ya lugha. Pamoja na hayo, vipengele vya wahusika na mandhari ni vya ziada katika ushairi. 1 Mtindo Tunapohakiki mtindo wa ushairi tunaangalia urari wa vina na mizani. Hapa tunapata aina za shairi ambazo ni la kisasa au la kimapokeo. Endapo shairi litafuata urari wa vina na mizani litakuwa la kimapokeo na lisipofuata basi ni la kisasa. Vina ni silabi za mwisho zinazofanana katika kipande. Mshororo mmoja una vi...