Ubantu wa Kiswahili
Kuna nadharia mbalimbali zinazozungumzia asili ya Kiswahili.
Moja ya nadharia hizo ni ile inayodai kuwa Kiswahili ni Kibantu. Nadharia hii
inaegemea zaidi vigezo vya ulinganishi baina ya Kiswahili na lugha zingine za
Kibantu. Vigezo hivyo huonesha mfanano wa Kiswahili na lugha za Kibantu kama
vifuatavyo;
Kwanza ni mfanano wa msamiati wa msingi. Lugha ya Kiswahili
na lugha zingine za Kibantu zimefanana sana katika msamiati hasa ule wa msingi.
Kwa mfano; Neno la Kiswahili mwana
linafanana na umwana (Kinyakyusa) na ng’wana – Kisukuma. Pia, neno jicho linafanana na iliso – Kizulu, eliiso –
Kiruri, liso – Kisukuma na elisho – Kihaya. Mfanano huu
unadhibitisha kuwa Kiswahili ni mojawapo ya lugha za Kibantu.
Vivyo hivyo, vitenzi vya Kiswahili na vya lugha zingine za
Kibantu vina miishilizi...