Sunday, September 27Kiswahili kitukuzwe!

Sarufi

Sarufi za Kiswahili

Mzizi katika Kiswahili Sanifu
Sarufi

Mzizi katika Kiswahili Sanifu

Dhana ya Mzizi Karibu tena katika makala yetu ya sarufi ya Kiswahili sanifu. Katika makala haya tutajadili kuhusu dhana ya mzizi. Ambapo maana ya mzizi na aina za mzizi zitajadiliwa. Nini maana ya mzizi? Mzizi una maanisha nini? Mzizi ni nini? Mzizi ni sehemu ya neno ambayo haiwezi kuchanganuliwa zaidi bila kupoteza uamilifu wake. Kuchanganuliwa kunamaanisha kuondoa viambishi. Kwa hiyo ili tuweze kupata mzizi wa neno, tunapaswa kuondoa viambishi vyote ambavyo vyaweza kuwa awali, kati au tamati, kisha sehemu inayobaki ndiyo huitwa mzizi wa neno. Tazama mfano ufuatao; Kula > ku + l + aMlo > m + l + oMlaji > m + l + a + jiUlaji > u + l + a + ji Katika mfano huo tunaona sehemu ya neno ambayo haibadiliki ni "l". Hivyo basi huo ndiyo mzizi wa maneno; kula, mlo, m...
Lugha na Sifa Zake
Sarufi

Lugha na Sifa Zake

Karibu tena katika mwendelezo wa makala za sarufi ya Kiswahili. Leo tutajadili kuhusu maana ya lugha na sifa zake. Kwa ujumla binadamu wote huwasiliana kwa kutumia lugha iwe ya ishara, ya mazungumzo au ya maandishi. Katika maisha ya kila siku, mwanadamu lazima atumie lugha katika kujenga jamii, kuibomoa, kuafikiana, kufarakana, kujenga uadui, kujenga uhusiano mwema, kufanya ibada n.k. Cha ajabu ni kwamba binadamu hata akiwa amelala hutumia lugha akiwa ndotoni, akihoji na kusikiliza hoja. Kwa mantiki hiyo, lugha ni chombo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Lugha ni nini? Wanaisimu hukubaliana kuwa lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zilizobeba maana na zilizochaguliwa na jamii fulani ili zitumike kwa makusudi ya kupashana habari au kuwasiliana. Hata hivyo, katika fasili hii tunaona k...
Vihusishi vya Kiswahili Sanifu
Sarufi

Vihusishi vya Kiswahili Sanifu

Karibu kwenye makala zetu za sarufi ya Kiswahili Sanifu. Katika makala ya leo tutajadili kuhusu kihusishi kama aina mojawapo ya maneno. Aina hii ya neno ni miongoni mwa aina kuu za maneno zinazojenga aina za virai. Aina zingine ni nomino, vitenzi, vivumishi na vielezi. Vihusishi ni aina ya neno ambayo inaonesha uhusiani uliopo baina ya neno moja na neno jingine katika tungo. Vihusishi vinaweza kuonesha umahali, utumizi, sababu, sehemu ya kitu kizima, ulinganifu au umiliki. Tazama mifano ifuatayo inayoonesha vihusishi. Juma ameenda kwa baba yake.Siwezi kula kwa kijiko hicho.Siku hiyo, baba alicheza na watoto wake.Alifeli kwa sababu yake.Walifungana mbili kwa tatu.Alichukua mbili ya tatu ya chungwa hilo.Waliongea kuhusu mashamba.Alifafanua kwa mujibu wa sheria.Walikuja kutoka Mbeya.Al...
Vihisishi/Viingizi Vya Kiswahili Sanifu
Sarufi

Vihisishi/Viingizi Vya Kiswahili Sanifu

Karibu tena katika mwendelezo wetu wa kujadili mada za sarufi ya Kiswahili Sanifu. Katika makala ya leo tutajadili kuhusu vihisishi au viingizi kama aina mojawapo ya maneno. Karibu sana. Kihisishi ni aina neno ambalo huonesha mguso wa ndani wa mzunguzaji kuhusu jambo alilolisikia au aliloliona. Vihusishi huweza kuonesha hisia au mguso wa woga, kushangaa, kuumia, kufurahi, kusononeka au uridhika. Sehemu nyingine kihisishi kimepewa jina la viingizi. Kwa maana hiyo, viingizi ni kisawe cha neno kihisishi. Pamoja na hayo, mifano ifuatayo inaonesha vihisishi; Alaaah! kumbe alishafia.Waoooo! tumefanikiwaa!Mama weee! nusura agongwe.Daah! kumbe ni yeye?Oyeee! sisi ni sisi. Kutokana na mifano hapo juu, maneno yaliyoandikwa kwa herufi mlalo ni vihisishi.
Viwakilishi vya Kiswahili Sanifu
Sarufi

Viwakilishi vya Kiswahili Sanifu

Karibu tena katika mwendelezo wa makala zetu za sarufi ya Kiswahili. Leo tunajadili kuhusu nini maana ya kiwakilishi? au kiwakilishi ni nini? aina za viwakilishi na tabia za viwakilishi. Kiwakilishi ni aina ya neno ambalo husimama badala ya nomino. Hii inamaanisha kuwa kiwakilishi husimama mahala ambapo nomino ingepaswa kusimama. Viwakilishi ni kama vile; huyu, yule, wewe, mimi, wao, sisi, ninyi, wale, kile n. k. Aina za Viwakilishi Kiwakilishi kioneshiKiwakilishi kiuliziKiwakilishi nafsiKiwakilishi rejeshiKiwakilishi cha idadiKiwakilishi kimilikishiKiwakilishi sifa Kiwakilishi Kioneshi Hiki ni kiwakilishi ambacho huonesha mahala kitu kilipo. Tazama mifano hapo chini. Kile kimeozaHawa ni wanafunzi wangu.Yule alimaliza chuo mwaka jana. Kutokana na mfano hapo juu, manen...
Viunganishi vya Kiswahili Sanifu
Sarufi

Viunganishi vya Kiswahili Sanifu

Karibu tena katika mwendelezo wa makala zetu za sarufi ya Kiswahili. Leo tutajadili kuhusu aina nyingine ya neno ambayo ni viunganishi vya Kiswahili Sanifu. Viunganishi ni maneno ambayo huweka pamoja vipashio vingine vyenye hadhi sawa. Vipashio hivyo ni kama vile neno na neno, kirai na kirai, kishazi na kishazi au sentensi na sentensi nyingine. Tazama mifano hapo chini kuhusu viunganishi. Mariam na Musa ni ndugu wa damu.Baba analima wakati mama anaandaa chakula cha jioni.Mtoto aliyevunjika mguu, amepelekwa hospitalini.Sikujisikia njaa wala uchovu.Alichukua viatu vyangu ingawa nilimkataza.Tanzania ni nchi ya Afrika Mashariki ilhali Sudani ni nchi ya Afrika ya Kati. Maneno yaliyoandikwa kwa herufi mlalo ni viunganishi. Katika mfano wa tatu hapo juu, tunaona kuwa sentensi imeunganis...
Vielezi vya Kiswahili Sanifu
Sarufi

Vielezi vya Kiswahili Sanifu

Karibu katika muendelezo wa aina za maneno zinazopatikana katika lugha ya Kiswahili. Hapa tutajadili kuhusu vielezi kama aina mojawapo ya maneno ya Kiswahili Sanifu. Vielezi ni aina ya maneno ambayo hutoa taarifa zaidi uhusu Vitenzi. Vielezi hutoa taarifa namna kitendo kilivyofanyika, sehemu kilipofanyikia, kilifanyika wakati gani na pia kilifanyika mara ngapi. Kutokana na hayo tunapata aina nne za vielezi ambazo ni; Vielezi vya Namna au jinsiVielezi vya MahaliVielezi vya Wakati naVielezi vya Idadi Aina hizi za vielezi zinaelezwa moja baada ya nyingine hapo chini. Vielezi ya Namna au Jinsi Hivi ni vielezi ambavyo hutoa taarifa kuhusu namna au jinsi kitendo kilivyofanyika. Kwa mfano, Juma anatembea taratibu.Musa huja kwa kujivuta vuta.Baba alisononeka sana.Gari moshi li...
Vivumishi vya Kiswahili Sanifu
Sarufi

Vivumishi vya Kiswahili Sanifu

Kisemantiki, kivumishi ni aina ya neno ambalo hueleza zaidi kuhusu nomino au kiwakilishi. Kwa kuwa kivumishi hueleza zaidi kuhusu aina hizo za maneno. Hivyo basi, vivumishi haviwezi kusimama katika sentensi pasina nomino au kiwakilishi. Kimofolojia, kivumishi ni aina ya neno ambalo hujengwa na kiambishi cha upatanishi pamoja na mzizi wa kivumishi. Kwa mfano. m - zuri, ki - zuri, ki - bovu n.k. Aina za Vivumishi Vivumishi huweza kuwekwa katika aina mbalimbali kama ifuatavyo: Vivumishi SifaVivumishi IdadiVivumishi VioneshiVivumishi Viulizi (vya Kuuliza)Vivumishi VimilikishiKivumishi Kirejeshi (Vivumishi Rejeshi) Vivumishi Sifa Hivi ni vivumishi viaevyoelezea zaidi kuhusu sifa ya nomino au kiwakilishi. Tazama mifano hapo chini inayoonesha aina ya vivumishi hivi: Mtoto...
Vitenzi vya Kiswahili Sanifu
Makala, Sarufi

Vitenzi vya Kiswahili Sanifu

Aina hii ya neno huweza kufafanuliwa kwa kutumia vigezo mbalimbali vya kiisimu ambavyo ni; kisemantiki, kimofolojia na kisintaksia. Hata hivyo maana inayotokana na semantiki ndiyo huegemewa zaidi. Tazama hapo chini namna ya kufasili kitenzi kwa kutumia vigezo mbalimbali. Kisemantiki, vitenzi ni aina ya neno inayotaja tendo au hali ya kuwa. Kwa mfano; ...
Nomino za Kiswahili Sanifu
Sarufi

Nomino za Kiswahili Sanifu

Nomino ni aina ya neno inayotaja majina ya vitu vilivyo hai na visivyo hai. i.e, wanyama, mahali, mimea na vitu visivyo wanyama wala mimea. Kwa mfano, mawe, Joni, kiazi, meli, sambusa, Dar es Salaam n.k. Aina za Nomino Kwa kutumia kigezo cha kisemantiki, kuna aina kuu tatu za nomino ambazo ni: Nomino za kawaida, nomino dhahania na nomino za pekee. A: Nomino za Kawaida hutaja majina ya vitu vya kawaida yasiyo mahususi au yanayotaja vitu kwa ujumla wake. Nomino huandikwa kwa kuanza na herufi ndogo isipokuwa mwanzoni mwa sentensi. Mfano wa nomino za kawaida ni kama nomino zinazotaja vitu, mahali, majina ya wanyama na mimea. Kwa mfano, nyumba, kompyuta, ngazi, ndani, mkoani, nje, nchi, mti, mtu, mchungwa, pilipili, sindano n.k. Nomino za kawaida hugawanywa katika aina kuu tatu. ...