Sunday, September 27Kiswahili kitukuzwe!

Nukuu Kidato cha nne

Pata nukuu za kidato cha Nne

Njia Mbalimbali za Kuunda Maneno
Nukuu Kidato cha nne

Njia Mbalimbali za Kuunda Maneno

Ili kukidhi haja ya mawasiliano jamii huunda maneno mapya. Maneno hayo huweza kuundwa kwa njia mbalimbali. Njia hizo ni kama zifuatazo; Uambishaji Hii ni njia ya uundaji wa maneno kwa kupachika viambishi mwanzoni au mwishoni mwa mzizi wa neno. Mzizi mmoja wa neno huweza kuzalisha neno zaidi ya moja. Tutazame mifano ifuatayo; mzizi lim- unaweza kuunda maneno; Kilimo, Mkulima na Lima.Mzizi chez- unaweza kuunda maneno; Cheza, Mchezaji, Mchezo na chezea.Mzizi pat- unaweza kuunda maneno; pata na kipato.Mzizi end- unaweza kuunda maneno; nenda, mwendo na endeshaMzizi funik- unaweza kuunda maneno; funika, mfuniko Pamoja na hayo, njia hii huweza kubadili aina ya neno. Kategoria huweza kutoka kitenzi kuwa nomino, nomino kuwa kielezi au kivumishi n.k. Kwa mfano kitenzi piga huweza kuwa...
KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI
Nukuu Kidato cha nne

KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI

Uundaji wa Maneno Jamii yoyote inapopata maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni huhitaji kuongeza misamiati mipya ili kukidhi haja ya mawasiliano. Kwa hiyo basi, njia mbalimbali za uundaji wa meneno hutumika ili kufikia adhma hiyo. Mazingira Yanayosababisha Kuhitaji Maneno Mapya Mabadiliko yoyote yanapotokea katika jamii, ni lazima maneno mapya yaundwe ili kukidhi haja ya mawasiliano. Kwa hiyo mazingira yanayosababisha uhitaji wa maneno mapya ni pamoja na; Mabadiliko ya kiutamaduni, mabadiliko ya kimazingira, mripuko wa magonjwa, uvumbuzi wa vitu mbalimbali, ugunduzi wa mambo mbalimbali,  mwingiliano wa kijamii na wakati. Mambo haya yanajadiliwa hapo chini. Jamii inapobadilika kiutamaduni, maneno mapya huundwa ili kukidhi haja ya mawasiliano. Kwa mfano mit...
MAENDELEO YA KISWAHILI
Nukuu Kidato cha nne

MAENDELEO YA KISWAHILI

UKUAJI NA UENEAJI WA KISWAHILI BAADA YA UHURU Kutokana na umuhimu wake wakati wa ukombozi, lugha ya Kiswahili ilipewa nafasi kubwa sana baada ya kupata uhuru. Serikali ilisaidia sana kukuza na kuenea Kiswahili baada ya uhuru kwa kufanya yafuatayo; Kiswahili Kupewa Hadhi ya Lugha ya Taifa Baada ya uhuru serikali ilitangaza kuwa Kiswahili kitakuwa lugha ya taifa. Kwa kuwa lugha hii iliunganisha watu mbalimbali nchini haikuwa shida kupokelewa na wananchi wengi. Kutokana na hili, lugha ya Kiswahili ilianza kutumika bungeni, katika ofisi za serikali, kwenye mikutano ya kijiji, shughuli zote za kisiasa, shuleni, sokoni, kwenye biashara mbalimbali na kila kona ya nchi. Jambo hili liliwafanya wananchi wengi wajifunze Kiswahili. Kiswahili Kutumika kama Lugha ya Kufundishia na Kam...
KUKUA NA KUENEA KWA KISWAHILI
Nukuu Kidato cha nne

KUKUA NA KUENEA KWA KISWAHILI

WAINGEREZA NA BAADA YA UHURU UKUAJI NA UENEAJI WA KISWAHILI KATIKA ENZI YA WAINGEREZA Bendera ya Tanganyika katika utawala wa Mwingereza Waingereza waliichukua Tanganyika chini ya utawala wa Wajerumani baada ya vita ya kwanza ya dunia mwaka 1918. Wakati huo Kiswahili kilikuwa kimeenea sana hata kufikia Kiwango cha kushinda matumizi ya lugha za kwanza nchini Tanganyika. Kutokana na jambo hilo, Waingereza hawakuwa na la kufanya ila kuendelea kutoka pale ambapo Wajerumani walipokuwa wameachia.  Kwa kuwa walitafuta urahisi wa kuwatawala Watanganyika, waliamua kutumia lugha moja inayotumiwa na wengi ili kuwapa elimu. Lugha hiyo ilikuwa Kiswahili. Kwa kufanya hivyo, walieneza na kukuza Kiswahili. Kwa namna hiyo, mambo yaliyosaidia kukuza na kueneza Kiswahili katika enzi ya Mwinger...