Monday, April 12Kiswahili kitukuzwe!

Michezo

Mpira wa Miguu – Soka
Entertainment, Makala, Michezo

Mpira wa Miguu – Soka

Mpira wa Miguu, maarufu kama soka, ni mchezo unaohusisha timu mbili za wachezaji 11, wakitumia sehemu za miili yao isipokuwa mikono, wakiuchezea mpira kutafuta kupenya goli la timu pinzani. Mlinda mlango pekee ndiye anaruhusiwa kushika mpira na anaweza kufanya hivyo tu ndani ya eneo la penalti kuzunguka goli. Timu inayofunga magoli mengi ndiyo inayoshinda. Mpira wa miguu ndiyo mchezo wa mpira maarufu na wenye mashabiki wengi na washiriki pia. Kwa ufupi katika miongozo ya msingi na vifaa mujimu, mchezo huo unaweza kuchezwa kokote, kwenye viwanja rasmi vya kuchezea, kumbi za michezo, mitaani, viwanja vya michezo vya shule na ufukweni. Shirikisho la soka Duniani Fédération Internationale de Football Association (FIFA) lilikadiria kuwa karne ya 21 kulikuwa na takribani wachezaji ...