Kishazi rejeshi
SINTAKSIA YA KISHAZI REJESHI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI.
Utangulizi; Sintaksia ya kishazi rejeshi ni moja kati ya maeneo ya sarufi ambayo yanatoa fursa nzuri ya kueleza jinsi nadharia ya sarufi-geuzi-zalishi inavyoweza kutoa maelezo toshelevu juu ya mchakato wa urejeshi katika lugha ya Kiswahili.
Kwanza ni vema itambulike kwamba kishazi rejeshi ni kishazi tegemezi ambacho hukumusha kirainomino ambacho tayari ni kijenzi ndani ya kishazi kikuu. Kwa mujibu wa kanuni za sintaksia ya Kiswahili kirainomino kinaweza kujitokeza katika nafasi zifuatazo katika sentensi ya Kiswahili;
KIIMA; Watoto waliimba mashairi jana.
Watoto walifundishwa vizuri jana.
YAMBWA; Watoto wanachuma maua bustanin...