Tuesday, August 4Kiswahili kitukuzwe!

Fasihi

Fasihi ya Kiswahili

Fasihi

Fasihi Kwa Ujumla

Karibu katika sehemu hii ya mjadala kuhusu fasihi. Kwa ujumla fasihi ni miongoni mwa sanaa zisizoweza kutengwa katika maisha ya kila siku ya mwanadamu. Fasihi huweza kutokea wakati wa sherehe, misiba, tambo, kazi za msarambo (zile zinazofanywa kwa kushirikiana), wakati wa kutoa maonyo na majuto. Kutokana na mambo hayo yote inaonekana kuwa fasihi na maisha ya mwanadamu ni kama pande mbili za shilingi. Hata hivyo, fasihi ni nini? swali hili linajibiwa hapo chini. Fasihi ni sanaa itumiayo lugha katika kufikisha ujumbe wake. Fasihi ni sanaa kwa kuwa hutumia ufundi katika kuwasilisha ujumbe kwa hadhira. Ufundi huo huonekana zaidi katika matumizi ya lugha ambapo lugha za kisanaa hutumika. Lugha hizo ni kama vile; mbaalagha, taswira, ishara, matumizi ya semi, nidaa, tashibiha, takriri, tashi...