Monday, April 12Kiswahili kitukuzwe!

Fasihi

Fasihi ya Kiswahili

Fasihi Simulizi; Nyambi
Fasihi

Fasihi Simulizi; Nyambi

Karibu tena katika mwendelezo wetu wa makala zinazohusu fasihi ya kiswahili Sanifu. Katika makala yetu ya leo tutajadili kuhusu nyambi. Ambapo tutaona maana yake pamoja na tanzu zake. Nyambi ni nini? Kwanza kabisa tanapaswa kutambua kuwa neno nyambi ni wingi ambapo umoja wake ni WAMBI. Sasa wambi ni nini? Wambi ni mzungumzo yaliyo na usanaa ndani yake. Huzingatia muktadha, muundo na mtiririko. Humfanya hadhira aendelee kusikiliza kwani huvutia na kuamsha msisimko fulani. Kama vile vicheko, hasira, shangwe n.k TANZU ZA WAMBI HotubaMalumbano ya wataniMizaha Maombi HOTUBA Hotuba ni mazungumzo rasmi yanayotolewa na mgeni rasmi kwa hadhira. Mazungumzo hayo hujawa vitendawili, misemo, simo na mbinu nyingi za kisanaa. Hotuba hutolewa sehemu rasmi na kwenye matukio rasmi kama...
Hadithi: Mapisi
Fasihi

Hadithi: Mapisi

Karibu tena katika makala yetu yanazohusu fasihi. Leo tutajadili kuhusu kipera kimojawapo cha hadithi simulizi ambacho ni mapisi. Hapa tutaeleza kuhusu maana ya mapisi, dhima zake, sifa aina za kipera hiki. Mapisi ni nini? Mapisi ni kipera cha hadithi ambacho husimulia matukio ya kihistoria yaani habari za mambo ya kale. Mapisi hueleza matukio kama yalivyotukia bila ya kuweka chuku au kwa kuweka chuku au ubunifu ndani yake. Dhima kubwa ya mapisi ni kutunza historia ya jamii fulani kuhusu matukio ya kishujaa au matukio maalumu yaliyoacha alama katika jamii husika. Sifa za Mapisi Hueleza matukio ya kihistoria.Huwa na ukweli ndani yake.Ni thibitivu, yaani mambo yanayoelezwa huweza kuthibitishwa.Hutunza historia ya jamii.Huweka kumbukumbu kuhusu kuhusu jamii ya watu fulani...
Hadithi: Kisasili
Fasihi

Hadithi: Kisasili

Karibu tena katika makala zetu za fasihi. Leo tutajadili kuhusu kipera kimojawapo cha hadithi simulizi ambacho ni Kisasili. Kwa hiyo tutaangalia maana, sifa na aina mbalimbali za visasili. Kisasili ni nini? Kisasili ni hadithi ya kale yenye kuwakilisha imani na mtazamo wa jamii kuhusu asili ya ulimwengu na mwenendo wake, asili ya jamii yenyewe na watu wake na maana ya maisha yao na vyote hivyo huaminika kuwa ni kweli tupu na huambatana na miviga (matendo ya kimila). Dhima kubwa ya kisasili ni kutetea imani ya kiroho inayofuatwa na na jamii. Kwa hiyo, kila jamii ina kisasili chake kinachoeleza kuhusu asili, chimbuko na mustakabali wa maisha yao. Jambo kubwa la kuweka wazi hapa ni kuwa kisasili huambatana na imani ya jamii na ya mtu mmoja mmoja. Imani ile ambayo uliapa kuilind...
Hadithi: Hekaya
Fasihi

Hadithi: Hekaya

Sungura mjanja Karibu tena katika makala zetu za fasihi ya Kiswahili. Leo tutajadili kuhusu tanzu mojawapo ya hadithi simulizi. Tanzu hiyo ni hekaya. Neno Hekaya humaanisha; kioja, ajabu au shani. Nini Maana ya Hekaya? Hekaya ni hadithi ya kimapokeo ambayo huwa na visa vya kusisimua na kustaajabisha vilivyojaa shani. Katika hadithi hizi huwa na wahusika wanjanja na wahusika majuha. Wahusika wanjanja hutumia ujanja wao ili kujinufaisha wenyewe. Mfano wa hekaya ni kama vile hadithi za Sungura na Fisi, Hekaya za Abunuasi na Hadithi za Alfu - Lela - Ulela Dhima kuu ya hekaya ni kusisimua na kuburudisha huku ikielezea matukio ya ajabu ambayo hujaa shani. Pia, hadithi hizi hufundisha kwa namna fulani wanajamii wawe wavumilivu au watu wanaofikiria sana.
Hadithi: Mchapo (Soga)
Fasihi

Hadithi: Mchapo (Soga)

Karibu tena katika makala zetu za fasihi ya Kiswahili. Katika makala ya leo tutajadili kuhusu mchapo kama tanzu mojawapo ya Hadithi. Mchapo pia hujulikana kama Soga. Kwa hiyo katika makala haya, tanzu mchapo itatumika kwa maana ile ile ya tanzu ya Soga. Nini maana ya Mchapo? au nini maana ya Soga? Mchapo/Soga ni utanzu wa fasihi simulizi unaosimulia kuhusu tukio fulani kwa kusudi la kusisimua na kufurahisha. Utanzu huu pia hutumika kama masimulizi yanayoibua utani kuhusu jamii fulani ya watu. Mfano wa mchapo ni kama vile; haditi zinazongumzia kwa nini Wahehe hula mbwa, Wasafya kula panya n.k. Tazama mfano hapo chini kuhusu fisi aitwaye Musa. Asili ya fisi huyo kuitwa Musa ni kwa vile siku moja alipojaribu kumkamata mwanamke aliyekuwa amelewa; bibi huyo alidhani fisi ni mu...
Hadithi
Fasihi

Hadithi

Karibu tena katika makala zetu za fasihi. Leo tutajadili kuhusiana na Hadithi kama utanzu wa fasihi simulizi. Hadithi ni utanzu unaobeba visa na matukio ya kweli au ya kubuni ili kuburudisha na kutoa ujumbe. Hadithi ni nini? Hadithi ni masimulizi ya lugha ya mjazo kuhusu visa na matukio mbalimbali yamhusuyo binadamu na jamii yake. Hadithi huwa na wahusika mbalimbali ambao ndiyo wafanyaji wa matendo yanayoibua visa fulani. Katika hadithi za fasihi simulizi kuna wahusika wanyama, binadamu, mimea, miungu, majini n.k. Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa hadithi huwa na wahusika binadamu na viumbe hai, visivyo hai na vya kufikirika. Hata hivyo, wahusika wote hao huwakilisha matendo ya binadamu ili kutoa funzo katika jamii husika. Sifa za Hadithi Hadithi zina sifa zifuatazo; Huelez...
Semi 2
Fasihi

Semi 2

Karibu tena katika makala zetu zinazohusu fasihi. Katika makala haya tutajadili kuhusu tanzu zingine za semi ambazo ni mafumbo na misemo. Tazu hizi zitajadiliwa moja baada ya nyingine kama ifuatavyo; 3. Mafumbo Mafumbo ni semi zilizofichwa maana ili zifichuliwe au ziwekwe wazi. Mafumbo huweza kuwa; chemsha bongo, fumbo jina, tabaini/vitatanishi mara nyingine huitwa mizungu. Chemsha bongo ni maswali ambayo yanahitaji tafakuri ili kuyajibu. Baadhi ya maswali hayo ni ya kimapokeo lakini mengine hubuniwa na msemaji kwa kuilenga hadhira fulani. Kwa mfano, mbele ya bata kuna bata nyuma ya bata kuna bata. Je kuna bata wangapi? Tabaini/Mizungu/Vitatanishi ni semi za ukinzani zinazokusudia kutoa ujumbe fulani. Kwa mfano, mweupe si mweupe, mweusi si mweusi, mkimbizi asiyekimbia. Fum...
Semi 1
Fasihi

Semi 1

Karibu kwenye mwendelezo wa makala zetu zinazohusu fasihi ya Kiswahili. Katika makala haya tutajadili kuhusu semi kama kumbo mojawapo ya fasihi simulizi. Semi ni uwingi wa neno usemi. Kama ilivyojadiliwa katika makala yaliyopita, usemi ni kauli fupi za kisanaa zilizobeba maana na ujumbe kwa jamii fulani. Maana ya Semi Semi ni kauli fupi za kisanaa zilizobeba maana na ujumbe kwa jamii fulani. Kwa mfano; Samaki mkunje angali mbichi, mwenda pole hajikwai, mpanda ngazi hushuka, kuku wangu ametagia mibani, wazungu wawili wachungula dirishani na elimu ni bahari. Tanzu za Semi Semi ina tanzu zifutazo; MethaliVitendawiliMafumbo na Misemo 1. Methali Methali ni usemi mfupi uliojaa busara ndani yake na unaodokeza mafunzo mazito yaliyotokana na tajriba ya jamii husika. Tazamz...
Tanzu za Fasihi Simulizi
Fasihi

Tanzu za Fasihi Simulizi

Karibu tena katika mwendelezo wa mjadala kuhusu fasihi. Leo tutajadili kuhusiana na kumbo za fasihi simulizi. Pamoja na kuwa wengi wamezoea kugawanya fasihi simulizi katika makundi manne yaani; Hadithi, Ushairi, Semi na Sanaa za Maonesho, katika mjadala wetu tutaenda zaidi ya hapo. Kwa kumrejelea Mulokozi katika kitabu cha Utangulizi wa Fasihi Simulizi ya Kiswahili (2017), tunapata kumbo nane za fasihi simulizi. Kumbo hizo ni; Semi, Nyambi, Maombi, Hadithi, Maigizo, Ushairi, Maghani na Ngomezi. Kumbo hizi zimegawanywa kwa kuzingatia vigezo vifuatayo; Umbile na tabia ya kazi.Muktadha wa uwasilishwaji au utendaji wake.Namna ya uwasilishwaji wake kwa hadhira.Dhima ya kazi hiyo kwa jamii. Kwa kifupi tuangalie maana ya kumbo hizo kama zinavyofafanuliwa hapo chini. Semi ni utungo au...
AINA ZA FASIHI
Fasihi

AINA ZA FASIHI

Karibu tena katika mwendelezo wetu wa mada za fasihi ya Kiswahili. Leo tutajadili kuhusu aina za fasihi na sifa za kila moja. Kuna aina mbili za fasihi ambazo ni; Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi. Aina hizi zinajadiliwa moja baada ya nyingine sehemu inayofuata. FASIHI SIMULIZI Fasihi Simulizi ni fasihi itumiayo lugha ya masimulizi ya mdomo ili kufikisha ujumbe wake kwa hadhira iliyokusudiwa. Kabla ya maendeleo na mabadiliko mbalimbali ya uhifadhi, fasihi hii haikuwekwa katika maandishi. Hata hivyo, kutokana na ukuaji wa kiteknolojia na mabadiliko mbalimbali ya kiuhifadhi, fasihi hii haiwezi kutambuliwa tu kwa kuegemea masimulizi ya mdomo bali kwa kuangalia sifa zingine za kifasihi simulizi hasa hasa mianzo na miisho ya kifomula, matumizi ya wahusika wa fasihi simulizi n.k. ...