Monday, April 12Kiswahili kitukuzwe!

UUNDAJI WA MANENO

Katika mada hii tutajadili kuhusu njia mbili za uundaji wa maneno ambazo ni njia ya uambishaji na njia ya unyumbulishaji. Ili kuweza kutambua vyema njia hizi hatuna budi kwanza kujadili kuhusu MOFIMU.

MOFIMU

Mofimu ni kipashio kidogo cha kimofolojia chenye maana kisarufi na kileksika. Hii ni sehemu ndogo kabisa ambayo haiwezi kuvunjwa au kugawanywa zaidi bila kupoteza uamilifu wake[1]. Kazi za mofimu ni kama vile;

 • Kuonyesha njeo (Wakati uliopo, ulipita na ujao) kwa mfano; alilima, analima, amelima, atalima. Kiambishi li, na, mena ta, huonesha njeo
 • Kuonesha nafsi. Kwa mfano; Ninakula, unakula, anakula. Kiambishi ni, u na a vinaonesha nafsi.
 • Kuonesha umoja au wingi. Kwa mfano mtu – watu, mkubwa – wakubwa, anaimba – wanaimba. Kiambishi m, a, na wa huonesha umoja na wingi
 • Kuonesha ukanushi kwa mfano; siji, haimbi, hautaki. Viambishi si na ha vinaonesha ukanushi.
 • Kuonesha uyakinishi. Kwa mfano; Nitaenda, anaimba, unataka, Viambishi ni, a na u vinaonesha uyakinifu,
 • Kuonesha urejeshi kwa mfano; aliyekula, kilichovunjika, vilivyonunuliwa, alimoingia, lililoanguka n.k. Viambishi ye, cho, vyo, mo na lo huonesha urejeshi.
 • Kuonesha upatanishi wa kisarufi kwa mfano anacheza, unacheza, kitavunjika n.k. Viambishi a, u na ki vinaonesha upatanishi wa kisarufi,
 • Kuonesha kauli za vitenzi Kwa mfano; Imbia, imbisha, imbika, imbwa. Viambishi i, ish, ik na whuonesha kauli za vitenzi.

AINA ZA MOFIMU

Mofimu imegawanyika katika aina mbili ambazo ni; Mofimu huru na Mofimu tegemezi.

Mofimu Huru

Mofimu huru ni ambazo husimama peke yake na kutoa maana ya kileksika[2]. Maana ya kileksika ni maana kamili ya neno. Kwa hiyo, mofimu huru huwa na hadhi ya neno. Mifano ya mofimu huru ni kama vile; baba, simba, samaki, mama, ugali, mafuta, maji, korosho, ndege, mali, sungurana maneno mengine ambayo hasimama peke yake pasina kuchukua viambishi mbalimbali.

Mofimu Tegemezi

Mofimu tegemezi ni ambazo haziwezi kusimama pekee na kutoa maana ya kileksika ila huwa na maana ya kisarufi. Maana za kisarufi ni kazi ya kiambishi katika neno husika. Kwa mfano; mofimu huweza kuonesha njeo, urejeshi, kauli za vitenzina uamilifu mwingine kama ulivyotajwa hapo juu. Tazama mifano hapo chini:

 1. A – li – tembe – a
 2. A – na – chez – a
 3. Wa – me – ku – l a
 4. Wa – toto
 5. Ha – wa – pig – an – i

Mifano hapo juu inaonesha mofimu tegemezi. Mofimu hizo zimetenganishwa na kistari. Kwa hiyo neno la kwanza lina mofimu nne, la pili mofimu nne, la tatu mofimu nne, la nne mofimu mbili na la tano lina mofimu tano. Kila mofimu hapo ina kazi yake, hata hivyo kazi hizo tutazijadili katika uambishaji.

1. UMBISHAJI  

Uambishaji ni njia ya uundaji wa maneno unaohususisha uongezaji wa viambishi mwanzoni, kati au mwishoni mwa mzizi wa neno. Uambishaji huzalisha maneno mengi kutoka katika mzizi mmoja. Tazama mifano hapo chini.

 1. – lim – huzaa; lima, mkulima, limisha, walimaji, kilimo, limia n.k
 2. – som – huzaa; soma, msomaji, wasomi, kisomo, somo, somea, somesha n.k.
 3. – imb – huzaa; imba, wimbo, imbisha, mwimbaji, nyimbo n.k.

Kutokana na mifano hapo juu sehemu iliyoandikwa kwa kukozwa ni mzizi wa neno.

Hata hivyo katika fasili ya umbishaji hapo juu, tunapata maneno mapya ambayo ni viambishi na mzizi. Maneno haya yanafasiliwa hapo chini.

VIAMBISHI

Umoja wa viambishi ni kiambishi. Kiambishi ni mofimu inayopachikwa mwanzoni, kati au mwishoni mwa mzizi wa neno.

Viambishi vina aina zake. Aina hizo hutokana nafasi kinamotokeza katika mzizi wa neno. Kwa namna hiyo kuna viambishi vya mwanzoni, vya katikati na vya mwishoni. Hii inafanya aina zifuatazo za viambiashi.

Kiambishi Awali

Kiambishi awali ni mofimu inayopachikwa mwanzoni mwa mzizi wa neno. Mwanzoni mwa mzizi wa neno ni upande wa kushoto kabla ya mzizi. Mifano wa viambishi awali ni kama ifuatayo.

 1. A – na lim – a
 2. Hapik – i
 3. Msom – i
 4. Ha – tu – ku – mkut – a
 5. Wa – na – m tukuz – a

Mofimu zilizoandikwa kwa mlalo ni viambishi awali.

Kazi za Viambishi Awali

 1. Huonesha nafsi
 2. Huonesha uyakinifu
 3. Huonesha ukanushi
 4. Huonesha umoja na wingi
 5. Huonesha njeo
 6. Huonesha urejeshi

Kiambishi Kati

Kiambishi kati ni mofimu inayopachikwa katikati ya mzizi wa neno. Katika lugha ya Kiswahili hakuna maneno yanayopokea viambishi kati kwa hiyo hakuna mifano ya Kiswahili ihusuyo viambishi hivyo.

Kiambishi Tamati  

Kiambishi tamati ni mofimu inayopachikwa mwishoni mwa mzizi wa neno. Mwishoni mwa mzizi wa neno ni upande wa kulia baada ya mzizi wa neno. Tazama mifano ifuatayo:

 1. Lim – ik – a
 2. Pig – an – a
 3. Chezesh – a
 4. Omba
 5. Zoe – lek – a

Mofimu zilizoandikwa kwa mlalo ni viamishi tamati.

Kwa kuwa katika lugha ya Kiswahili hakuna kiambishi kati, hivyo basi lugha hii ina viambishi awali na viambishi tamati tu.

Kazi ya Viambishi Tamati

 1. Huonesha maana
 2. Huonesha kauli mbalimbali za vitenzi
 3. Hubadili kategoria ya neno

Mzizi

Ni sehemu ya neno inayobaki baada ya kuondoa viambishi awali na viambishi tamati. Kwa namna nyingine ni mofimu inayobaki baada ya kupachua viambishi awali na viambishi tamati. Mzizi hauwezi kuvunjwa zaidi na ukaleta maana. Hata hivyo mzizi mmoja huweza kuzalisha maneno mengi. Tazama mifano ifuatayo;

 1. Sal – a,
 2. Sal – ish – a
 3. Sal – i
 4. Chez – a
 5. Chez – an – a
 6. Chez – w – a

Sehemu iliyoandikwa kwa kukozwa ni mzizi wa neno.


[1] Uamilifu ni kazi ifanywayo na kipashio.

[2] Leksimu ni kisawe cha neno.

2. UNYAMBULISHAJI

Unyambulishaji ni kitendo cha kuongeza viambishi tamati katika mzizi wa neno ili kulitanua neno. Kitendo cha neno kunyumbulika huitwa mnyumbuliko. Kwa hiyo, unyambulishaji ni moja kati ya aina za uambishaji.

Kwa kuwa unyambulishaji ni kitendo cha kunyumbua maneno kwa kuyaongezea viambishi tamati, hivyo basi kaida hii huthibitika hasa katika kauli za vitenzi. Tazama mifano ifuatayo;

 1. Lima = limia, limika, limisha
 2. Cheza = chezeka, chezeana, chezwa
 3. Soma = somea, someka, somesha
 4. Chora = chorea, choreka, choresha
 5. Linda = lindwa, lindika, lindia

Tutazame mifano zaidi ya kauli za vitenzi katika jedwali lifuatalo.

TendaTendanaTendeaTendeanaTendwaTendewaTendekaTendeshaTendeshwaTendeshea
Oaoanaoleaoleanaolewa    –olekaozeshaozeshwaozeshea
Imbaimbanaimbiaimbianaimbwaimbiwaimbikaimbishaimbishwaimbishia
Rukarukanarukiarukianarukwarukiwarukikarukisharukishwarukishia
Cheza*Chezanachezeachezeanachezwachezewachezekachezeshachezeshwachezeshea
Ombaombanaombeaombeanaombwaombewaombekaombeshaombeshwaombeshea
Limalimanalimialimianalimwalimiwalimikalimishalimishwalimishia
andikaandikanaandikiaandikianaandikwaandikiwaandikikaandikishaamdikishwaandikishia

Kubadili Kategoria (aina) ya Neno kwa Kutumia Uambishaji

Tunaweza kubadili aina ya neno kwa kuongeza mofimu katika neno chanzi. Tazama mifano hapo chini.

Nomino kuwa Kitenzi

NominoMziziKitenzi
WimboImb –Imba
NominoMziziKitenzi
SomoSom –Soma
KilimoKil –Lima
SalaSal –Sali
MchezoChez –Cheza
OmbiOmb –Omba
UsemiSem –Sema

Nomino kuwa Kielezi

NominoMziziKielezi
ShambaShamba –Shambani
MkonoKono –Mkononi
shingoShingo-shingoni

Nomino kuwa Kivumishi

NoninoMziziKivumishi
UshujaaShujaaKijana shujaa
UkwelikweliMtoto mkweli
UvivuvivuMwanafuni mvivu

Kivumishi kuwa Kielezi

KivumishiMziziKielezi
– mvivuvivukivivu
– shujaashujaakishujaa
– mtaratibutaratibukiutaratibu

40 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *