Monday, April 12Kiswahili kitukuzwe!

Day: March 29, 2021

UTATA KATIKA TUNGO
Makala, Nukuu Kidato cha Pili

UTATA KATIKA TUNGO

Nini maana ya Utata? Utata ni hali ya tungo kuwa na maana zaidi ya moja. Neno au sentensi yenye utata hutatanisha kimaana yaani haieleweki kwa yakini humaanisha hivi au vile? Tazama mifano hapo chini; Nenda ukanichukulie mbuzi. Swali: Mbuzi mnyama au mbuzi kifaa cha kukunia nazi? Juma anapanda. Swali: Juma anakwea au anaotesha mbegu? Ile nyumba ni ya wageni Swali: Ni nyumba ya kulala wageni au nyumba inamilikiwa na wageni? Mtoto amelalia uji. Swali: Amelala juu ya uji au hakula kitu kingine zaidi ya uji kisha akalala? Mwajuma ametumwa na Rama. Swali: Aliyemtuma Mwajuma ni Rama au Mwajuma na Rama wametumwa? Sababu za Kutokea kwa Utata Neno au sentensi kuwa na maana zaidi ya moja. Matumizi ya neno au sentensi yenye maana za moja huleta utata. Ma...