Monday, April 12Kiswahili kitukuzwe!

Day: March 6, 2021

UUNDAJI WA MANENO
Makala, Nukuu Kidato cha Pili

UUNDAJI WA MANENO

Katika mada hii tutajadili kuhusu njia mbili za uundaji wa maneno ambazo ni njia ya uambishaji na njia ya unyumbulishaji. Ili kuweza kutambua vyema njia hizi hatuna budi kwanza kujadili kuhusu MOFIMU. MOFIMU Mofimu ni kipashio kidogo cha kimofolojia chenye maana kisarufi na kileksika. Hii ni sehemu ndogo kabisa ambayo haiwezi kuvunjwa au kugawanywa zaidi bila kupoteza uamilifu wake[1]. Kazi za mofimu ni kama vile; Kuonyesha njeo (Wakati uliopo, ulipita na ujao) kwa mfano; alilima, analima, amelima, atalima. Kiambishi li, na, mena ta, huonesha njeoKuonesha nafsi. Kwa mfano; Ninakula, unakula, anakula. Kiambishi ni, u na a vinaonesha nafsi.Kuonesha umoja au wingi. Kwa mfano mtu – watu, mkubwa – wakubwa, anaimba – wanaimba. Kiambishi m, a, na wa huonesha umoja na wingiKuonesha ukanu...