Mjengo wa Tungo
Karibu tena katika makala zetu zinazojikita katika kutoa maarifa ya kiswahili kwa kidato cha tatu. Leo tutajadili kuhusu namna tungo zinavyojengwa katika lugha.
Tungo ni nini?
Tungo ni kipashio cha kimuundo ambacho hutokana na uwekwaji pamoja wa vipashio vidogo ili kuunda kipashio kikubwa zaidi. Tungo huweza kutoa taarifa kamili au isiyo kamili.
Kimuundo kuna aina nne za tungo ambazo ni; tungo neno, tungo kirai, tungo kishazi na tungo sentensi. Mpangilio huu umeanza na tungo ya chini kabisa hadi tungo ya juu kabisa. Hivyo, neno hujenga kirai, kirai hujenga kishazi na kishazi hujenga sentensi. Angalia zaidi ufafanuzi hapo chini.
Tungo Neno
Neno ni kipashio kidogo kabisa cha kimuundo kilichoachiwa nafasi pande zote mbili na hutoa maana. Katika Kiswahili kuna aina mbalimbali ...