Monday, April 12Kiswahili kitukuzwe!

UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI

Karibu tena katika makala zetu zilizojikita kutoa maarifa ya Kiswahili kwa kidato cha tatu. Katika makala ya leo tutajadili kuhusu Uhakiki wa kazi za Fasihi Andishi. Ambapo tutaanagalia maana ya uhakiki na vipengele vyake.

Katika kuchunguza uhakiki wa kazi za fasihi andishi tunapaswa kujua dhana mbalimbali zinazohusiana na uhakiki. Dhana hizo ni uhakiki, mhakiki na tahakiki. Basi na tuangalie dhana hizo moja baada ya nyingine.

 1. Uhakiki ni kitendo cha kuchambua na kufafanua vipengele vya fani na maudhui vinavyojenga fasihi.
 2. Mhakiki ni mtu anayechambua na kufafanua vipengele vya fani na maudhui vinavyojenga fasihi.
 3. Tahakiki ni kitabu kinachochambua vipengele vya fani na maudhui.

FANI

ni nui au ufundi anaoutumia msanii wa fasihi katika kuwasilisha mawazo yake. Tunaweza kusema pia, fani ni namna msanii anavyowasilisha mawazo (Maudhui) yake.

Fani imejengwa na vipengele vifuatavyo;

 1. Wahusika
 2. Mandhari
 3. Muundo
 4. Mtindo
 5. Matumizi ya lugha

MAUDHUI

Ni jumla ya mawazo yote ya mwandishi katika kazi ya fasihi. Maudhui hujumuisha vipengele vifuatavyo;

 1.  dhamira
 2. ujumbe
 3. migogoro.
 4. falsafa na
 5. mtazamo

Katika makala yajayo tutajadili kuhusu vipengele vinavyojenga fani na maudhui kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *