Tuesday, August 4Kiswahili kitukuzwe!

Day: August 1, 2020

UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI
Makala, Nukuu Kidato cha Tatu

UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI

Karibu tena katika makala zetu zilizojikita kutoa maarifa ya Kiswahili kwa kidato cha tatu. Katika makala ya leo tutajadili kuhusu Uhakiki wa kazi za Fasihi Andishi. Ambapo tutaanagalia maana ya uhakiki na vipengele vyake. Katika kuchunguza uhakiki wa kazi za fasihi andishi tunapaswa kujua dhana mbalimbali zinazohusiana na uhakiki. Dhana hizo ni uhakiki, mhakiki na tahakiki. Basi na tuangalie dhana hizo moja baada ya nyingine. Uhakiki ni kitendo cha kuchambua na kufafanua vipengele vya fani na maudhui vinavyojenga fasihi.Mhakiki ni mtu anayechambua na kufafanua vipengele vya fani na maudhui vinavyojenga fasihi.Tahakiki ni kitabu kinachochambua vipengele vya fani na maudhui. FANI ni nui au ufundi anaoutumia msanii wa fasihi katika kuwasilisha mawazo yake. Tunaweza kusema pia, f...