UHAKIKI WA RIWAYA 2
Karibu tena katika mwendelezo wa makala haya yanayojikita katika kutoa maarifa ya Kiswahili kwa kidato cha tatu. Leo tutashughulika na uchambuzi wa riwaya ya Joka la Mdimu. Ambapo vipengele vya fani na maudhui vinajadiliwa kama ifuatavyo;
JINA LA KITABU: Joka la Mdimu
MWANDISHI: Abdallah J. Saffari
Utangulizi
Riwaya hii inaakisi matatizo ya kiuchumi yanayoikumba jamii. Msanii ameweza kuonesha namna wananchi wanavyopata shida katika kupata huduma za kijamii kama vile; usafiri, matibabu, mavazi, makazi n.k.
Pia, msanii amaeonesha matabaka. Katika jamii kuna tabaka tawala na tabaka tawaliwa. Tabaka tawala linaonekana kuwa na maisha bora zaidi wakati tabaka tawaliwa lina maisha ya taabu yaliyojaa dhiki.
Kutokana na hali ngumu ya maisha, wananchi wa tabaka la chini wanaji...