Sunday, September 27Kiswahili kitukuzwe!

Fasihi Simulizi; Nyambi

Karibu tena katika mwendelezo wetu wa makala zinazohusu fasihi ya kiswahili Sanifu. Katika makala yetu ya leo tutajadili kuhusu nyambi. Ambapo tutaona maana yake pamoja na tanzu zake.

Nyambi ni nini?

Kwanza kabisa tanapaswa kutambua kuwa neno nyambi ni wingi ambapo umoja wake ni WAMBI. Sasa wambi ni nini?

Wambi ni mzungumzo yaliyo na usanaa ndani yake. Huzingatia muktadha, muundo na mtiririko. Humfanya hadhira aendelee kusikiliza kwani huvutia na kuamsha msisimko fulani. Kama vile vicheko, hasira, shangwe n.k

TANZU ZA WAMBI

  1. Hotuba
  2. Malumbano ya watani
  3. Mizaha
  4. Maombi

HOTUBA

Hotuba ni mazungumzo rasmi yanayotolewa na mgeni rasmi kwa hadhira. Mazungumzo hayo hujawa vitendawili, misemo, simo na mbinu nyingi za kisanaa. Hotuba hutolewa sehemu rasmi na kwenye matukio rasmi kama vile; vikao vya kimila, kidini, kisiasa n.k.

Hotuba hutolewa na watu rasmi wenye ujuzi wa lugha husika. Mhutubiaji hutumia mbinu za kisanaa ili kuvuta hisia za wasikilizaji.

Usanii wa hutuba hutokana na; uigizaji wa matukio, matumizi ya jazanda na kutumia lugha ya mvuto.

UTANI

Utani ni maneno waambianayo watu ili kuchekeshana. Huwa na kanuni zake na una mipaka. Huonesha uhusiano wa wahusika. Pia, utani huwa na pande mbili zinazotaniana.

Kunaweza kuwa na utani wa makabila, bibi/babu na wajukuu, mashemeji, marafiki au wa marika.

MZAHA

Mzaha ni masimulizi mafupi ya kuchekesha yaliyojaa kebehi ndani yake. Mzaha husaili tabia ya kijinga ya mtu au ya jamii fulani. Pia, mizaha inaweza kuambatana na matusi ndani yake.

Dhima ya mzaha ni kufurahisha na kuchekesha hadhira hasa wawapo katika mazingira ambayo siyo rasmi.

Kisawe cha mzaha ni SOGA au MICHAPO

MAOMBI

Ni matendo ya kusaka msaada wa kiungu kutokana na changamoto zinazomkumba mwanadamu. Lugha ya kisanaa hutumika wakati wa kufanya maombi, pia ushairi pamoja na matendo ya kuigiza hutumika.

Vipera vya Maombi

  1. Sala
  2. Dua
  3. Tambizi
  4. Tabano
  5. Maapizo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *