Tuesday, October 20Kiswahili kitukuzwe!

Day: May 6, 2020

Hadithi na masimulizi
Nukuu Kidato cha nne

Hadithi na masimulizi

Karibu tena katika makala zetu zinazoweza saidia wanafunzi wa kidato cha nne na wengineo. Leo tunajadili kuhusu hadithi za fasihi simulizi. Ambapo tutaona maana ya hadithi na vipera vyake pamoja na mifano ya hadithi hizo. Hadithi ni nini? Hii ni tanzu ya fasihi simulizi ambayo inahusisha masimulizi yaliyojengwa na visa pamoja na matukio mbalimbali. Hadithi huweza kuwa fupi au ndefu. Vivyo hivyo tanzu hii ina wahusika ambao ambao hubeba visa na matendo yamuwakilishayo mwanadamu. Wahusika wanaweza kuwa wanyama, binadamu, mimea, mizimu, miungu n.k. Tanzu hii ina vipera vitano ambavyo ni: Soga, Tarihi, Visasili, Ngano na Vigano. Vipera hivi vinafafanuliwa kimoja baada ya kingine hapo chini. SOGA Hizi ni hadithi fupi zenye ucheshi ambazo zinasimuliwa kwa nia ya kufanya mzaha. H...