Monday, April 12Kiswahili kitukuzwe!

UUNDAJI WA MANENO KATIKA MIKTADHA MBALIMBALI

Karibu katika makale zetu za nukuu za kitado cha nne. Leo tutajadili kuhusu uundaji wa maneno mapya katika miktadha mbalimbali.

Maneno mapya yanaweza kuunda katika miktadha ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kisayansi na kiutamaduni. Maneno hayo huundwa katika miktadha hii ili yaweze kuendana na mabadiliko yanayotokea katika jamii. Hapa chini kuna mifano ya maneno yaliyoundwa ili kukidhi miktadha hii.

Katika muktadha wa kiuchumi, maneno kama; ushuru, kodi, pesa, wakala, mteja, uza, nunua, soko, benki, marupurupu, kaunta na bidhaa hukidhi haja katika kufanikisha shughuli za kiuchumi.

Pia, katika muktadha wa sayansi na teknolojia, maneno kama; mashine, kompyuta (ngamizi), kikokotozi, saa, gari, ndege, barabara, reli, meli, runinga, redio nk. hukidhi haja ya mawasiliano ya kisayansi na kiteknolojia.

Vivyo hivyo, katika muktadha wa kisiasa maneno kama; bunge, utawala, sheria, rais, jamhuri, nchi, kitongoji, mwenyekiti, diwani n.k hukidhi haja ya kiutawala.

Si hivyo tu bali katika muktadha wa kijamii maneno kama; shule, hospitali, barabara, kisima, mwanaume, vita, ugali, mbilimbi n.k yameundwa ili kukidhi haja ya mawasiliano kijamii.

Mwisho katika muktadha wa kiutamaduni, maneno kama; ngoma, sherehe, sarakasi, tambiko, miiko, kabila, lugha, mila, desturi na ndoa hukidhi mawasiliano ya kijadi.

Tafadhali soma makala zilizopita zinazohusu njia za uundaji wa maneno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *