Sunday, September 27Kiswahili kitukuzwe!

Uandishi: Kumbukumbu za Mkutano

Karibu tena katika makala zetu za nukuu za kidato cha nne. Leo tutajadili kuhusu uandishi wa kumbukumbu za mikutano.

Kuandika na kutunza kumbukumbu za mikutano hutusaidia katika ufuatiliaji na utekelezaji wa mambo yaliyojadiliwa katika mikutano. Mwandishi anatakiwa awe na stadi za kusikiliza na aweze kufupisha yaliyokubaliwa katika maandishi. Katika kumbukumbu za mikutano mambo yanayoandikwa ni yale yaliyokubaliwa tu. 

Mambo Muhimu ya Kuzingatia katika Uandishi wa Kumbukumbu za Mikutano

 1. Kichwa cha Kumbukumbu

Kinatakiwa kioneshe mambo yafuatayo kwa ufupi; Mkutano unahusu nini, Mahali ulipofanyika na tarehe uliyofanyika.

2. Mahudhurio

Mwandishi anatakiwa kuonesha kipengele hiki katika sehemu kuu tatu:

 • Waliohudhuria

Hii ni orodha ya majina ya watu waliofika kwenye mkutano. Uandishi wa orodha hufuata nyadhifa au vyeo vya washiriki wa mkutano.  Kuanzia mwenyekiti, katibu, mwekahazina, n.k.

 • Waliotoa Udhuru (Maadhura)

Hii ni orodha ya majina ya wote waliopaswa kuwapo katika mkutano lakini wametoa taarifa za kutofika katika mkutano kutokana na sababu mbalimbali.

 • Wasiohudhuria

Hii ni orodha ya majina ya watu waliopaswa kufika katika mkutano lakini hawakuhudhuria bila ya kutoa taarifa yoyote.

3. Ajenda

Ni orodha ya mambo yaliyozungumzwa kwenye mkutano. Ajenda huandikwa kwa kifupi na huorodheshwa kwa kutumia vichwa. Pia, kama mkutano si wa mara ya kwanza huwa na kipengele cha yatokanayo. Yatokanayo hueleza makubaliano yote yaliyoafikiwa katika mkutano uliopita. 

4. Kufungua Mkutano

Mwenyekiti ndiye anayefungua mkutano na katibu hupaswa kuandika muda ambao mkutano ulifunguliwa.

5. Mengineyo

Haya ni mambo mengine yanayojadiliwa nje ya ajenda zilizoandaliwa.

6. Kufunga Mkutano

Mwenyekiti ndiye hufunga mkutano. Mwandishi atapaswa kuandika muda au saa mkutano ulipofungwa.

Angalizo:

 • Lugha inayotumika katika uandishi wa kumbukumbu za mikutano huwa katika wakati uliopita, huandikwa kwa usemi wa taarifa, katika kauli ya kutendwa na hutumia nafsi ya tatu.
 • Katika uandishi wa kumbukumbu, maoni ya kundi zima hujumuishwa na si kwa majina ya watu waliotoa mchango ya mawazo, hoja au ushauri.

Mfano wa Kumbukumbu ya Mkutano

KUMBUKUMBU ZA MKUTANO WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA SHULE KUANZIA SAA 4:00 ASUBUHI HADI SAA 6:00 MCHANA TAREHE 25/08/2013 KUHUSU MAHAFALI ITAKAYOFANYIKA TAREHE 16/09/2013.

 1. Mahudhurio
  • Waliohudhuria
  • Waliotoa Hudhuru
  • Wasiohudhuria
 2. Ajenda
  • Kufungua Mkutano
  • Uchaguzi wa Viongozi
  • Sare
  • Chakula na Vinywaji
  • Mengineyo

3. Kufunga Mkutano

Mwenyekiti alifungua mkutano mnamo saa 4:00 asubuhi. Na kuwaeleza wajumbe madhumuni ya mkutano huo.

4. Uchaguzi wa Viongozi

Wajumbe walichagua viongozi ambao wataongoza katika kamati ya mahafali. Viongozi waliochaguliwa ni Juma Maligani ambaye ni mwenyekiti, Neema Mtunduru (Katibu), Moses Ntapa (Mwekahazina) na Roza Lambuka (mshereheshaji). Viongozi hao waliridhia nafasi hizo na kuwashukuru wajumbe kwa kuonesha imani kwao.

5. Sare

Wajumbe walikubaliana kuwa, sare ambayo itatumika katika mahafali ni shati jeupe na suti ya bluu. Ambapo suti hiyo itakuwa suruali kwa wavulana na sketi kwa wasichana. Pia, walikubaliana kuvaa tai za vipepeo, viatu vyeusi na soksi nyeupe kwa wasichana na nyeusi kwa wavulana. Sare hii itagharamiwa na mhitimu mwenyewe.

6. Chakula na Vinywaji

Wajumbe walikubaliana kuwa, chakula cha sherehe ya mahafali kigharamiwe na wote ambao watahudhuria mahafali hayo. Hivyo, kila mhitimu atachangia kiasi cha shilingi elfu 20. Waalikwa wengine, wakiwemo kidato cha kwanza hadi cha tatu, wachangie shilingi elfu 10. Pia, watakao saidia katika kuandaa chakula hicho ni wasichana wa kidato cha tatu.

7. Mengineyo

Wajumbe walikubaliana kuwa katika mahafali hayo, kuwe na michezo mbalimbali kama vile kwaya na maonesho ya vipaji mbalimbali. Mambo haya yatasaidia kuleta msisimko wa sherehe.  

8. Kufunga Mkutano

Mwenyekiti aliahirisha kikao mnamo saa 6:00 mchana na kuahidiana kukutana katika kikao kifuatacho tarehe 04/09/2013.

 Imedhibitishwa na

Mwenyekiti……………………………….…  Tarehe……………        Katibu………………..…………..     Tarehe……..…….

4 Comments

 • Howdy, i read your blog occasionally and i own a similar one
  and i was just wondering if you get a lot
  of spam responses? If so how do you protect against it, any plugin or
  anything you can advise? I get so much lately it’s driving me insane so any help is very much appreciated.

 • With havin so much content and articles do you ever
  run into any problems of plagorism or copyright infringement?

  My site has a lot of exclusive content I’ve either created
  myself or outsourced but it appears a lot of it is popping it
  up all over the internet without my authorization. Do you know any techniques to help stop content from being ripped off?

  I’d certainly appreciate it.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *