Sunday, September 27Kiswahili kitukuzwe!

Nadharia ya Uhakiki wa Ushairi

Ushairi
Uandishi wa ushairi Picha na Pixabay

Ili kuhakiki ushairi tunatumia vipengele vya fani na maudhui kama ilivyo katika kazi zingine za kisanaa.

MAUDHUI

Hapa tunachunguza vipengele kama vile; dhamira, ujumbe, falsafa, mtazamo na migogoro. Vipengele hivi vinasaidia kuelimisha jamii.

FANI

Tunajikita katika kuchunguza; Mtindo, muundo, wahusika, mandhari na matumizi ya lugha. Pamoja na hayo, vipengele vya wahusika na mandhari ni vya ziada katika ushairi.

1 Mtindo

Tunapohakiki mtindo wa ushairi tunaangalia urari wa vina na mizani. Hapa tunapata aina za shairi ambazo ni la kisasa au la kimapokeo. Endapo shairi litafuata urari wa vina na mizani litakuwa la kimapokeo na lisipofuata basi ni la kisasa.

Vina ni silabi za mwisho zinazofanana katika kipande. Mshororo mmoja una vipande viwili hivyo kuna kina cha kati na kina cha mwisho.

Mizani ni idadi ya silabi katika mshororo mmoja. Kwa utaratibu ushairi wa kimapokeo huwa na mizani 16 yaani nane kwa kila kipande.

2 Muundo

Muundo wa ushairi huhakikiwa kwa kuangalia idadi ya mishororo kwa kila ubeti. Kwa hiyo katika muundo tunapata aina zifuatazo za mashairi;

  • Tamolitha ni shairi lenye mstari mmoja kwa kila ubeti.
  • Tathnia ni shairi mistari miwili kwa kila ubeti.
  • Tathilitha ni shairi lenye mistari mitatu kwa kila ubeti.
  • Tarbia ni shairi lenye mistari minne kwa kila ubeti.
  • Takhimisa/Sabilia ni shairi lenye mistari mitano na kuendelea kwa kila ubeti.

3 Matumizi ya Lugha

Matumizi ya tamathali za semi na mbinu zingine za kisanaa kama vile sitiari, mubaalagha, tashibiha, takriri n.k

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *