Friday, July 10Kiswahili kitukuzwe!

Day: April 23, 2020

Muhtasari wa Uchambuzi wa Diwani ya Malenga Wapya na Wasakatonge
Nukuu Kidato cha nne

Muhtasari wa Uchambuzi wa Diwani ya Malenga Wapya na Wasakatonge

Jina la Kitabu: Wasakatonge Mwandishi: Mohammed S Khatibu Utangulizi Diwani hii imejikita katika kutetea tabaka la wasionacho. Tabaka hili linanyanyaswa, linakandamizwa na kuonewa na tabaka la walionacho. Kwa ujumla mwandishi anataka kujenga jamii mpya ambayo itakuwa na usawa na inayozingatia misingi ya haki. MAUDHUI Dhamira Kuu Katika diwani hii tunapata dhamira kuu mbili ambazo ni; Ujenzi wa Jamii mpya naUkombozi. Ujenzi wa Jamii Mpya Mwandishi anajadili ujenzi wa jamii mpya ambayo inatupilia mbali unyonyaji, unafiki, matabaka, uongozi mbaya na usaliti. Kwa hiyo mwandishi anaona kuwa tutaifikia jamii mpya kwa; Kupiga Vita Uongozi mbaya Uongozi mbaya ni chanzo cha matatizo katika jamii. Uongozi mbaya hunyima wananchi haki na hukandamiza wanyonge. Jamii ...
Nadharia ya Uhakiki wa Ushairi
Nukuu Kidato cha nne

Nadharia ya Uhakiki wa Ushairi

Uandishi wa ushairi Picha na Pixabay Ili kuhakiki ushairi tunatumia vipengele vya fani na maudhui kama ilivyo katika kazi zingine za kisanaa. MAUDHUI Hapa tunachunguza vipengele kama vile; dhamira, ujumbe, falsafa, mtazamo na migogoro. Vipengele hivi vinasaidia kuelimisha jamii. FANI Tunajikita katika kuchunguza; Mtindo, muundo, wahusika, mandhari na matumizi ya lugha. Pamoja na hayo, vipengele vya wahusika na mandhari ni vya ziada katika ushairi. 1 Mtindo Tunapohakiki mtindo wa ushairi tunaangalia urari wa vina na mizani. Hapa tunapata aina za shairi ambazo ni la kisasa au la kimapokeo. Endapo shairi litafuata urari wa vina na mizani litakuwa la kimapokeo na lisipofuata basi ni la kisasa. Vina ni silabi za mwisho zinazofanana katika kipande. Mshororo mmoja una vi...
Ubantu wa Kiswahili
Makala, Nukuu Kidato cha nne

Ubantu wa Kiswahili

Kuna nadharia mbalimbali zinazozungumzia asili ya Kiswahili. Moja ya nadharia hizo ni ile inayodai kuwa Kiswahili ni Kibantu. Nadharia hii inaegemea zaidi vigezo vya ulinganishi baina ya Kiswahili na lugha zingine za Kibantu. Vigezo hivyo huonesha mfanano wa Kiswahili na lugha za Kibantu kama vifuatavyo; Kwanza ni mfanano wa msamiati wa msingi. Lugha ya Kiswahili na lugha zingine za Kibantu zimefanana sana katika msamiati hasa ule wa msingi. Kwa mfano; Neno la Kiswahili mwana linafanana na umwana (Kinyakyusa) na ng’wana – Kisukuma. Pia, neno jicho linafanana na iliso – Kizulu, eliiso – Kiruri, liso – Kisukuma na elisho – Kihaya. Mfanano huu unadhibitisha kuwa Kiswahili ni mojawapo ya lugha za Kibantu. Vivyo hivyo, vitenzi vya Kiswahili na vya lugha zingine za Kibantu vina miishilizi...