Friday, July 10Kiswahili kitukuzwe!

Day: April 20, 2020

Uandishi: Kumbukumbu za Mkutano
Nukuu Kidato cha nne

Uandishi: Kumbukumbu za Mkutano

Karibu tena katika makala zetu za nukuu za kidato cha nne. Leo tutajadili kuhusu uandishi wa kumbukumbu za mikutano. Kuandika na kutunza kumbukumbu za mikutano hutusaidia katika ufuatiliaji na utekelezaji wa mambo yaliyojadiliwa katika mikutano. Mwandishi anatakiwa awe na stadi za kusikiliza na aweze kufupisha yaliyokubaliwa katika maandishi. Katika kumbukumbu za mikutano mambo yanayoandikwa ni yale yaliyokubaliwa tu.  Mambo Muhimu ya Kuzingatia katika Uandishi wa Kumbukumbu za Mikutano Kichwa cha Kumbukumbu Kinatakiwa kioneshe mambo yafuatayo kwa ufupi; Mkutano unahusu nini, Mahali ulipofanyika na tarehe uliyofanyika. 2. Mahudhurio Mwandishi anatakiwa kuonesha kipengele hiki katika sehemu kuu tatu: Waliohudhuria Hii ni orodha ya majina ya watu waliofik...
Uandishi wa Risala
Nukuu Kidato cha nne

Uandishi wa Risala

Karibu tena katikata makala zetu zinazohusu nukuu za kidato cha nne. Leo tajikita katika uandishi wa risala. Risala ni nini? Risala ni maelezo maalumu yanayotolewa na kikundi cha watu kwenda kwa mgeni rasmi. Pamoja na kuwa risala humlenga mgeni rasmi lakini lengo kuu huwa hadhira inayohusika kupata ujumbe. Mara nyingi risala husomwa katika matukio mbalimbali ya kijamii hasa sherehe. Muundo wa Risala Kichwa cha Risala Sehemu hii hutaja kusudi la risala na kikundi au wahusika walioandaa risala hiyo. Kichwa cha risala huandikwa kwa herufi kubwa, hupigiwa mstari au kukolezwa.   Mwanzo wa risala Sehemu hii ni utambulisho, humtaja mgeni rasmi, viongozi na halaiki kwa kuzingatia nyadhifa zao. Pia, hutaja madhumuni ya risala. Kiini cha Risala Hapa ndipo maudhui y...
Uandishi wa Hotuba
Nukuu Kidato cha nne

Uandishi wa Hotuba

Karibu tena katika makala zetu za nukuu za kidato cha nne. Leo tutajadili kuhusu uandishi wa hotuba. Hotuba ni nini? Hotuba ni maelezo maalumu yanayotolewa na mtu mbele ya kundi la watu kwa madhumuni maalumu. Hotuba huweza kuwa za mafundisho au za taarifa. Hotuba za mafundisho ni kama vile; mahubiri au mawaidha, kampeni za kisiasa juu ya sera mbalimbali za vyama n.k. Hotuba za taarifa ni kama vile ripoti ya wizara au za kitaaluma. Mambo ya kuzingatia wakati wa uandishi wa Hotuba. Hotuba lazima ieleze ukweli kuhusu jambo au taarifa inayotolewaLugha fasaha itumikeIwe imepangiliwa kimantikiIwapo kuna matumizi ya ishara lazima zitumike ipasavyoSauti ya mtoa hotuba lazima isikike Muundo wa Hotuba Utangulizi Katika sehemu hii kuna salamu kwa jumla na kuwatambua watu muhim...
Makala, Nukuu Kidato cha nne

LAHAJA ZA KISWAHILI

Karibu tena katika makala zetu zinazoegemea nukuu za kidato cha nne. Leo tutajadili kuhusu lahaja za Kiswahili Sanifu. Lahaja ni nini? Lahaja ni uzungumzaji tofauti wa lugha moja. Lahaja za lugha moja hutofautiana kimatamshi, kimiundo na kimsamiati.  Hizi hutokea katika lugha yoyote yenye wazungumzaji wengi. Kiswahili ni moja kati ya lugha ambazo zina wazungumzaji wengi. Kutokana na hili lugha hii ina lahaja nyingi. Mfano wa lahaja za Kiswahili ni Kimtang’ata, Kingazija, Kimvita, Kigwana n.k. AINA ZA LAHAJA Lahaja zinaweza kugawanywa katika aina tatu ambazo ni: Lahaja za Kijiografia / Kitarafa Hizi ni lahaja ambazo hujinasibisha na mahali. Kutokana na lahaja hizi tunatambua mahali mtu atokako. Kwa mfano; Lahaja ya Kiunguja hupatikana Unguja, Kimgao – Kilwa, Kiam...
Nukuu Kidato cha nne

UUNDAJI WA MANENO KATIKA MIKTADHA MBALIMBALI

Karibu katika makale zetu za nukuu za kitado cha nne. Leo tutajadili kuhusu uundaji wa maneno mapya katika miktadha mbalimbali. Maneno mapya yanaweza kuunda katika miktadha ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kisayansi na kiutamaduni. Maneno hayo huundwa katika miktadha hii ili yaweze kuendana na mabadiliko yanayotokea katika jamii. Hapa chini kuna mifano ya maneno yaliyoundwa ili kukidhi miktadha hii. Katika muktadha wa kiuchumi, maneno kama; ushuru, kodi, pesa, wakala, mteja, uza, nunua, soko, benki, marupurupu, kaunta na bidhaa hukidhi haja katika kufanikisha shughuli za kiuchumi. Pia, katika muktadha wa sayansi na teknolojia, maneno kama; mashine, kompyuta (ngamizi), kikokotozi, saa, gari, ndege, barabara, reli, meli, runinga, redio nk. hukidhi haja ya mawasiliano ya kisayansi n...
Nukuu Kidato cha nne

Njia za Kuunda Maneno mapya

Karibu tena katika mwendelezo wa makala zetu zanazohusu nukuu za kidato cha nne. Leo tutaangalia tanaendelea kujadili njia nyingine za uundaji wa maneno. KUBADILI MPANGILIO WA MANENO Njia hii huhusika katika ubadilishaji wa mpangilio wa herufi katika neno ili kuundwa neno jipya au maneno mapya. Mifano ifuatayo inaonesha hilo; Neno Imla linaweza kuwa; Mila, lima, mali au lamiNeno tatu linaweza kuwa; tuta, utata au tatua Neno tiba linaweza kuwa; bati, tabiaNeno kali linaweza kuwa; lika, alika, kalia URUDUFISHAJI/URADIDI Hii ni njia nyingine ya uundaji wa meneno ambapo neno jipya huundwa kwa kurudiarudia neno moja. Hapa nenio linalorudiwa ni neno amilifu yaani linalojitosheleza kimaana likiwa pekeyake. Tazama mifano ifuatayo: sawa →sawasawambali→  mbalimbaliPole→  Polepole...