Friday, July 10Kiswahili kitukuzwe!

Day: April 18, 2020

Nukuu Kidato cha nne

Njia Mbalimbali za Kuunda Maneno

Ili kukidhi haja ya mawasiliano jamii huunda maneno mapya. Maneno hayo huweza kuundwa kwa njia mbalimbali. Njia hizo ni kama zifuatazo; Uambishaji Hii ni njia ya uundaji wa maneno kwa kupachika viambishi mwanzoni au mwishoni mwa mzizi wa neno. Mzizi mmoja wa neno huweza kuzalisha neno zaidi ya moja. Tutazame mifano ifuatayo; mzizi lim- unaweza kuunda maneno; Kilimo, Mkulima na Lima.Mzizi chez- unaweza kuunda maneno; Cheza, Mchezaji, Mchezo na chezea.Mzizi pat- unaweza kuunda maneno; pata na kipato.Mzizi end- unaweza kuunda maneno; nenda, mwendo na endeshaMzizi funik- unaweza kuunda maneno; funika, mfuniko Pamoja na hayo, njia hii huweza kubadili aina ya neno. Kategoria huweza kutoka kitenzi kuwa nomino, nomino kuwa kielezi au kivumishi n.k. Kwa mfano kitenzi piga huweza kuwa...
Nukuu Kidato cha nne

KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI

Uundaji wa Maneno Jamii yoyote inapopata maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni huhitaji kuongeza misamiati mipya ili kukidhi haja ya mawasiliano. Kwa hiyo basi, njia mbalimbali za uundaji wa meneno hutumika ili kufikia adhma hiyo. Mazingira Yanayosababisha Kuhitaji Maneno Mapya Mabadiliko yoyote yanapotokea katika jamii, ni lazima maneno mapya yaundwe ili kukidhi haja ya mawasiliano. Kwa hiyo mazingira yanayosababisha uhitaji wa maneno mapya ni pamoja na; Mabadiliko ya kiutamaduni, mabadiliko ya kimazingira, mripuko wa magonjwa, uvumbuzi wa vitu mbalimbali, ugunduzi wa mambo mbalimbali,  mwingiliano wa kijamii na wakati. Mambo haya yanajadiliwa hapo chini. Jamii inapobadilika kiutamaduni, maneno mapya huundwa ili kukidhi haja ya mawasiliano. Kwa mfano mitindo ...