Friday, July 10Kiswahili kitukuzwe!

Day: April 6, 2020

Nukuu Kidato cha nne

MAENDELEO YA KISWAHILI

UKUAJI NA UENEAJI WA KISWAHILI BAADA YA UHURU Kutokana na umuhimu wake wakati wa ukombozi, lugha ya Kiswahili ilipewa nafasi kubwa sana baada ya kupata uhuru. Serikali ilisaidia sana kukuza na kuenea Kiswahili baada ya uhuru kwa kufanya yafuatayo; Kiswahili Kupewa Hadhi ya Lugha ya Taifa Baada ya uhuru serikali ilitangaza kuwa Kiswahili kitakuwa lugha ya taifa. Kwa kuwa lugha hii iliunganisha watu mbalimbali nchini haikuwa shida kupokelewa na wananchi wengi. Kutokana na hili, lugha ya Kiswahili ilianza kutumika bungeni, katika ofisi za serikali, kwenye mikutano ya kijiji, shughuli zote za kisiasa, shuleni, sokoni, kwenye biashara mbalimbali na kila kona ya nchi. Jambo hili liliwafanya wananchi wengi wajifunze Kiswahili. Kiswahili Kutumika kama Lugha ya Kufundishia na Kam...