Friday, July 10Kiswahili kitukuzwe!

Day: April 5, 2020

Nukuu Kidato cha nne

KUKUA NA KUENEA KWA KISWAHILI

WAINGEREZA NA BAADA YA UHURU UKUAJI NA UENEAJI WA KISWAHILI KATIKA ENZI YA WAINGEREZA Bendera ya Tanganyika katika utawala wa Mwingereza Waingereza waliichukua Tanganyika chini ya utawala wa Wajerumani baada ya vita ya kwanza ya dunia mwaka 1918. Wakati huo Kiswahili kilikuwa kimeenea sana hata kufikia Kiwango cha kushinda matumizi ya lugha za kwanza nchini Tanganyika. Kutokana na jambo hilo, Waingereza hawakuwa na la kufanya ila kuendelea kutoka pale ambapo Wajerumani walipokuwa wameachia.  Kwa kuwa walitafuta urahisi wa kuwatawala Watanganyika, waliamua kutumia lugha moja inayotumiwa na wengi ili kuwapa elimu. Lugha hiyo ilikuwa Kiswahili. Kwa kufanya hivyo, walieneza na kukuza Kiswahili. Kwa namna hiyo, mambo yaliyosaidia kukuza na kueneza Kiswahili katika enzi ya Mwinger...