Friday, July 10Kiswahili kitukuzwe!

Month: March 2020

Sarufi

Mzizi katika Kiswahili Sanifu

Dhana ya Mzizi Karibu tena katika makala yetu ya sarufi ya Kiswahili sanifu. Katika makala haya tutajadili kuhusu dhana ya mzizi. Ambapo maana ya mzizi na aina za mzizi zitajadiliwa. Nini maana ya mzizi? Mzizi una maanisha nini? Mzizi ni nini? Mzizi ni sehemu ya neno ambayo haiwezi kuchanganuliwa zaidi bila kupoteza uamilifu wake. Kuchanganuliwa kunamaanisha kuondoa viambishi. Kwa hiyo ili tuweze kupata mzizi wa neno, tunapaswa kuondoa viambishi vyote ambavyo vyaweza kuwa awali, kati au tamati, kisha sehemu inayobaki ndiyo huitwa mzizi wa neno. Tazama mfano ufuatao; Kula > ku + l + aMlo > m + l + oMlaji > m + l + a + jiUlaji > u + l + a + ji Katika mfano huo tunaona sehemu ya neno ambayo haibadiliki ni "l". Hivyo basi huo ndiyo mzizi wa maneno; kula, mlo, m...
Fasihi

Hadithi: Mapisi

Karibu tena katika makala yetu yanazohusu fasihi. Leo tutajadili kuhusu kipera kimojawapo cha hadithi simulizi ambacho ni mapisi. Hapa tutaeleza kuhusu maana ya mapisi, dhima zake, sifa aina za kipera hiki. Mapisi ni nini? Mapisi ni kipera cha hadithi ambacho husimulia matukio ya kihistoria yaani habari za mambo ya kale. Mapisi hueleza matukio kama yalivyotukia bila ya kuweka chuku au kwa kuweka chuku au ubunifu ndani yake. Dhima kubwa ya mapisi ni kutunza historia ya jamii fulani kuhusu matukio ya kishujaa au matukio maalumu yaliyoacha alama katika jamii husika. Sifa za Mapisi Hueleza matukio ya kihistoria.Huwa na ukweli ndani yake.Ni thibitivu, yaani mambo yanayoelezwa huweza kuthibitishwa.Hutunza historia ya jamii.Huweka kumbukumbu kuhusu kuhusu jamii ya watu fulani...
Fasihi

Hadithi: Kisasili

Karibu tena katika makala zetu za fasihi. Leo tutajadili kuhusu kipera kimojawapo cha hadithi simulizi ambacho ni Kisasili. Kwa hiyo tutaangalia maana, sifa na aina mbalimbali za visasili. Kisasili ni nini? Kisasili ni hadithi ya kale yenye kuwakilisha imani na mtazamo wa jamii kuhusu asili ya ulimwengu na mwenendo wake, asili ya jamii yenyewe na watu wake na maana ya maisha yao na vyote hivyo huaminika kuwa ni kweli tupu na huambatana na miviga (matendo ya kimila). Dhima kubwa ya kisasili ni kutetea imani ya kiroho inayofuatwa na na jamii. Kwa hiyo, kila jamii ina kisasili chake kinachoeleza kuhusu asili, chimbuko na mustakabali wa maisha yao. Jambo kubwa la kuweka wazi hapa ni kuwa kisasili huambatana na imani ya jamii na ya mtu mmoja mmoja. Imani ile ambayo uliapa kuilind...