Monday, April 12Kiswahili kitukuzwe!

Hadithi

Karibu tena katika makala zetu za fasihi. Leo tutajadili kuhusiana na Hadithi kama utanzu wa fasihi simulizi. Hadithi ni utanzu unaobeba visa na matukio ya kweli au ya kubuni ili kuburudisha na kutoa ujumbe.

Hadithi ni nini?

Hadithi ni masimulizi ya lugha ya mjazo kuhusu visa na matukio mbalimbali yamhusuyo binadamu na jamii yake. Hadithi huwa na wahusika mbalimbali ambao ndiyo wafanyaji wa matendo yanayoibua visa fulani. Katika hadithi za fasihi simulizi kuna wahusika wanyama, binadamu, mimea, miungu, majini n.k. Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa hadithi huwa na wahusika binadamu na viumbe hai, visivyo hai na vya kufikirika. Hata hivyo, wahusika wote hao huwakilisha matendo ya binadamu ili kutoa funzo katika jamii husika.

Sifa za Hadithi

Hadithi zina sifa zifuatazo;

  1. Hueleza matukio katika mpangilio mahsusi.
  2. Huwa na wahusika.
  3. Ina lugha ya mjazo.
  4. Uwasilishwaji wake huambatana na matendo pamoja na ishara.
  5. Huwa na maudhui ya kweli au ya kubuni.
  6. Huwa na mianzo na miisho ya kifomula i.e. Paukwa…! , Pakawa..!

Tanzu na vipera vya Hadithi

Utanzu Vipera
Ngano a) Istara
b) Kisasuli
c) Hurafa
d) Mbazi
Mchapo  
Hekaya  
Kisasili a) Cha Kabila/Taifa
b) Cha Miungu
c) Cha Usuli
d) Cha dini/Ibada
Kisakale  
Mapisi a) Salua
b) Tarihi
c) Shajari
d) Nasabu

Pamoja na kuwa tanzu za hadithi simulizi zilizozoeleka ni; ngano, visasili, vigano na tarihi lakini mgawanyo huo hapo juu umezama zaidi. Tanzu hizo zitaelezwa moja baada ya nyingine katika makala zifuatazo.

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *