Monday, April 12Kiswahili kitukuzwe!

Hadithi: Mchapo (Soga)

Karibu tena katika makala zetu za fasihi ya Kiswahili. Katika makala ya leo tutajadili kuhusu mchapo kama tanzu mojawapo ya Hadithi. Mchapo pia hujulikana kama Soga. Kwa hiyo katika makala haya, tanzu mchapo itatumika kwa maana ile ile ya tanzu ya Soga.

Nini maana ya Mchapo? au nini maana ya Soga?

Mchapo/Soga ni utanzu wa fasihi simulizi unaosimulia kuhusu tukio fulani kwa kusudi la kusisimua na kufurahisha. Utanzu huu pia hutumika kama masimulizi yanayoibua utani kuhusu jamii fulani ya watu.

Mfano wa mchapo ni kama vile; haditi zinazongumzia kwa nini Wahehe hula mbwa, Wasafya kula panya n.k. Tazama mfano hapo chini kuhusu fisi aitwaye Musa.

Asili ya fisi huyo kuitwa Musa ni kwa vile siku moja alipojaribu kumkamata mwanamke aliyekuwa amelewa; bibi huyo alidhani fisi ni mumewe aitwaye Musa, hata akamwita kwa sauti kuu, “Musa! Musa! Bwana wangu silewi tena bwana! Usiniadhibu namna hii, kwanza makucha yako leo makali bwana.” Basi watu walipokwenda kutazama ugomvi huu wa Musa na mkewe wakakuta yule fisi akijaribu kumvutia yule bibi mlevi maporini. Basi tangu siku ile fisi huyo akaitwa Musa.

Fisi Musa

Basi siku nyingine fisi huyo hupata akilia usiku katika kijiji cha Mikwanga. Wenyeji wakimsikia humjibu kwa maneno haya. “Musa! Musa! Bure wajisumbua, mpenzi wako halewi siku hizi, heri uende zako ukamtafute mchumba mwingine.”

Kwa ujumla, dhima kuu ya mchapo ni kuburudisha na kusisimua wakati wa mazungumzo yasiyo rasmi. Hata hivyo, kuna baadhi ya michapo huwa na ujumbe fulani.

38 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *