Monday, April 12Kiswahili kitukuzwe!

Hadithi: Hekaya

Sungura mjanja

Karibu tena katika makala zetu za fasihi ya Kiswahili. Leo tutajadili kuhusu tanzu mojawapo ya hadithi simulizi. Tanzu hiyo ni hekaya. Neno Hekaya humaanisha; kioja, ajabu au shani.

Nini Maana ya Hekaya?

Hekaya ni hadithi ya kimapokeo ambayo huwa na visa vya kusisimua na kustaajabisha vilivyojaa shani. Katika hadithi hizi huwa na wahusika wanjanja na wahusika majuha. Wahusika wanjanja hutumia ujanja wao ili kujinufaisha wenyewe.

Mfano wa hekaya ni kama vile hadithi za Sungura na Fisi, Hekaya za Abunuasi na Hadithi za Alfu – Lela – Ulela

Dhima kuu ya hekaya ni kusisimua na kuburudisha huku ikielezea matukio ya ajabu ambayo hujaa shani. Pia, hadithi hizi hufundisha kwa namna fulani wanajamii wawe wavumilivu au watu wanaofikiria sana.

5 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *