Sunday, July 5Kiswahili kitukuzwe!

Day: December 24, 2019

Fasihi

Hadithi: Hekaya

Sungura mjanja Karibu tena katika makala zetu za fasihi ya Kiswahili. Leo tutajadili kuhusu tanzu mojawapo ya hadithi simulizi. Tanzu hiyo ni hekaya. Neno Hekaya humaanisha; kioja, ajabu au shani. Nini Maana ya Hekaya? Hekaya ni hadithi ya kimapokeo ambayo huwa na visa vya kusisimua na kustaajabisha vilivyojaa shani. Katika hadithi hizi huwa na wahusika wanjanja na wahusika majuha. Wahusika wanjanja hutumia ujanja wao ili kujinufaisha wenyewe. Mfano wa hekaya ni kama vile hadithi za Sungura na Fisi, Hekaya za Abunuasi na Hadithi za Alfu - Lela - Ulela Dhima kuu ya hekaya ni kusisimua na kuburudisha huku ikielezea matukio ya ajabu ambayo hujaa shani. Pia, hadithi hizi hufundisha kwa namna fulani wanajamii wawe wavumilivu au watu wanaofikiria sana.
Fasihi

Hadithi: Mchapo (Soga)

Karibu tena katika makala zetu za fasihi ya Kiswahili. Katika makala ya leo tutajadili kuhusu mchapo kama tanzu mojawapo ya Hadithi. Mchapo pia hujulikana kama Soga. Kwa hiyo katika makala haya, tanzu mchapo itatumika kwa maana ile ile ya tanzu ya Soga. Nini maana ya Mchapo? au nini maana ya Soga? Mchapo/Soga ni utanzu wa fasihi simulizi unaosimulia kuhusu tukio fulani kwa kusudi la kusisimua na kufurahisha. Utanzu huu pia hutumika kama masimulizi yanayoibua utani kuhusu jamii fulani ya watu. Mfano wa mchapo ni kama vile; haditi zinazongumzia kwa nini Wahehe hula mbwa, Wasafya kula panya n.k. Tazama mfano hapo chini kuhusu fisi aitwaye Musa. Asili ya fisi huyo kuitwa Musa ni kwa vile siku moja alipojaribu kumkamata mwanamke aliyekuwa amelewa; bibi huyo alidhani fisi ni mu...