Sunday, July 5Kiswahili kitukuzwe!

Day: December 21, 2019

Makala

Hadithi: Ngano

Sindelera Karibu tena katika makala zetu zinazohusu fasihi ya Kiswahili. Katika makala ya leo tutajadili kuhusu tanzu mojawapo ya hadithi. Tanzu hiyo ni Ngano. Ngano ni nini? Ngano ni hadithi ya kimapokeo ambayo huelezea kisa cha wahusika wema na waovu ambapo mwishoni tunaona mhusika mwema anashinda. Mfano mzuri wa hadithi hizi ni kisa cha Sindelera.Ngano ni hadithi ambayo huwa na wahusika wa aina mbalimbali kama vile binadamu, wanyama, mizimu, mimea n.k. Hata hivyo wahusika hao huwakilisha matendo ya binadamu. Kwa kawaida ngano husimuliwa na wazazi, walezi, mabibi au mababu kwa watoto au wajukuu wao kwa lengo la kuwafunza vyema na kuwaburudisha. Kusudi kubwa la hadithi za kategoria hii ni kuelimisha jamii kwa kuonesha namna mwovu anavyopata adhabu. Pia, kukemea tabia zote...