Friday, July 10Kiswahili kitukuzwe!

Month: November 2019

Fasihi

AINA ZA FASIHI

Karibu tena katika mwendelezo wetu wa mada za fasihi ya Kiswahili. Leo tutajadili kuhusu aina za fasihi na sifa za kila moja. Kuna aina mbili za fasihi ambazo ni; Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi. Aina hizi zinajadiliwa moja baada ya nyingine sehemu inayofuata. FASIHI SIMULIZI Fasihi Simulizi ni fasihi itumiayo lugha ya masimulizi ya mdomo ili kufikisha ujumbe wake kwa hadhira iliyokusudiwa. Kabla ya maendeleo na mabadiliko mbalimbali ya uhifadhi, fasihi hii haikuwekwa katika maandishi. Hata hivyo, kutokana na ukuaji wa kiteknolojia na mabadiliko mbalimbali ya kiuhifadhi, fasihi hii haiwezi kutambuliwa tu kwa kuegemea masimulizi ya mdomo bali kwa kuangalia sifa zingine za kifasihi simulizi hasa hasa mianzo na miisho ya kifomula, matumizi ya wahusika wa fasihi simulizi n.k. ...