Sunday, September 27Kiswahili kitukuzwe!

Vihusishi vya Kiswahili Sanifu

Karibu kwenye makala zetu za sarufi ya Kiswahili Sanifu. Katika makala ya leo tutajadili kuhusu kihusishi kama aina mojawapo ya maneno. Aina hii ya neno ni miongoni mwa aina kuu za maneno zinazojenga aina za virai. Aina zingine ni nomino, vitenzi, vivumishi na vielezi.

Vihusishi ni aina ya neno ambayo inaonesha uhusiani uliopo baina ya neno moja na neno jingine katika tungo. Vihusishi vinaweza kuonesha umahali, utumizi, sababu, sehemu ya kitu kizima, ulinganifu au umiliki. Tazama mifano ifuatayo inayoonesha vihusishi.

 1. Juma ameenda kwa baba yake.
 2. Siwezi kula kwa kijiko hicho.
 3. Siku hiyo, baba alicheza na watoto wake.
 4. Alifeli kwa sababu yake.
 5. Walifungana mbili kwa tatu.
 6. Alichukua mbili ya tatu ya chungwa hilo.
 7. Waliongea kuhusu mashamba.
 8. Alifafanua kwa mujibu wa sheria.
 9. Walikuja kutoka Mbeya.
 10. Alimpiga kwa fimbo.
 11. Mintarafu ya ujumbe wako, sitarudia tena kuchelewa.

Kutokana na mifano hapo juu. Maneno yanayoonesha vihusishi ni; kwa, na, mintarafu, kutoka, kuhusu, pamoja na neno ya ambayo yameandikwa kwa herufi mlalo katika sentensi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *