Monday, January 25Kiswahili kitukuzwe!

Vihisishi/Viingizi Vya Kiswahili Sanifu

Karibu tena katika mwendelezo wetu wa kujadili mada za sarufi ya Kiswahili Sanifu. Katika makala ya leo tutajadili kuhusu vihisishi au viingizi kama aina mojawapo ya maneno. Karibu sana.

Kihisishi ni aina neno ambalo huonesha mguso wa ndani wa mzunguzaji kuhusu jambo alilolisikia au aliloliona. Vihusishi huweza kuonesha hisia au mguso wa woga, kushangaa, kuumia, kufurahi, kusononeka au uridhika.

Sehemu nyingine kihisishi kimepewa jina la viingizi. Kwa maana hiyo, viingizi ni kisawe cha neno kihisishi. Pamoja na hayo, mifano ifuatayo inaonesha vihisishi;

  1. Alaaah! kumbe alishafia.
  2. Waoooo! tumefanikiwaa!
  3. Mama weee! nusura agongwe.
  4. Daah! kumbe ni yeye?
  5. Oyeee! sisi ni sisi.

Kutokana na mifano hapo juu, maneno yaliyoandikwa kwa herufi mlalo ni vihisishi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *