Sunday, July 5Kiswahili kitukuzwe!

Day: October 20, 2019

Sarufi

Lugha na Sifa Zake

Karibu tena katika mwendelezo wa makala za sarufi ya Kiswahili. Leo tutajadili kuhusu maana ya lugha na sifa zake. Kwa ujumla binadamu wote huwasiliana kwa kutumia lugha iwe ya ishara, ya mazungumzo au ya maandishi. Katika maisha ya kila siku, mwanadamu lazima atumie lugha katika kujenga jamii, kuibomoa, kuafikiana, kufarakana, kujenga uadui, kujenga uhusiano mwema, kufanya ibada n.k. Cha ajabu ni kwamba binadamu hata akiwa amelala hutumia lugha akiwa ndotoni, akihoji na kusikiliza hoja. Kwa mantiki hiyo, lugha ni chombo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Lugha ni nini? Wanaisimu hukubaliana kuwa lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zilizobeba maana na zilizochaguliwa na jamii fulani ili zitumike kwa makusudi ya kupashana habari au kuwasiliana. Hata hivyo, katika fasili hii tunaona k...