Sunday, July 5Kiswahili kitukuzwe!

Day: October 11, 2019

Sarufi

Viwakilishi vya Kiswahili Sanifu

Karibu tena katika mwendelezo wa makala zetu za sarufi ya Kiswahili. Leo tunajadili kuhusu nini maana ya kiwakilishi? au kiwakilishi ni nini? aina za viwakilishi na tabia za viwakilishi. Kiwakilishi ni aina ya neno ambalo husimama badala ya nomino. Hii inamaanisha kuwa kiwakilishi husimama mahala ambapo nomino ingepaswa kusimama. Viwakilishi ni kama vile; huyu, yule, wewe, mimi, wao, sisi, ninyi, wale, kile n. k. Aina za Viwakilishi Kiwakilishi kioneshiKiwakilishi kiuliziKiwakilishi nafsiKiwakilishi rejeshiKiwakilishi cha idadiKiwakilishi kimilikishiKiwakilishi sifa Kiwakilishi Kioneshi Hiki ni kiwakilishi ambacho huonesha mahala kitu kilipo. Tazama mifano hapo chini. Kile kimeozaHawa ni wanafunzi wangu.Yule alimaliza chuo mwaka jana. Kutokana na mfano hapo juu, manen...