Sunday, July 5Kiswahili kitukuzwe!

Day: October 9, 2019

Sarufi

Viunganishi vya Kiswahili Sanifu

Karibu tena katika mwendelezo wa makala zetu za sarufi ya Kiswahili. Leo tutajadili kuhusu aina nyingine ya neno ambayo ni viunganishi vya Kiswahili Sanifu. Viunganishi ni maneno ambayo huweka pamoja vipashio vingine vyenye hadhi sawa. Vipashio hivyo ni kama vile neno na neno, kirai na kirai, kishazi na kishazi au sentensi na sentensi nyingine. Tazama mifano hapo chini kuhusu viunganishi. Mariam na Musa ni ndugu wa damu.Baba analima wakati mama anaandaa chakula cha jioni.Mtoto aliyevunjika mguu, amepelekwa hospitalini.Sikujisikia njaa wala uchovu.Alichukua viatu vyangu ingawa nilimkataza.Tanzania ni nchi ya Afrika Mashariki ilhali Sudani ni nchi ya Afrika ya Kati. Maneno yaliyoandikwa kwa herufi mlalo ni viunganishi. Katika mfano wa tatu hapo juu, tunaona kuwa sentensi imeunganis...