Sunday, July 5Kiswahili kitukuzwe!

Day: October 2, 2019

Sarufi

Vielezi vya Kiswahili Sanifu

Karibu katika muendelezo wa aina za maneno zinazopatikana katika lugha ya Kiswahili. Hapa tutajadili kuhusu vielezi kama aina mojawapo ya maneno ya Kiswahili Sanifu. Vielezi ni aina ya maneno ambayo hutoa taarifa zaidi uhusu Vitenzi. Vielezi hutoa taarifa namna kitendo kilivyofanyika, sehemu kilipofanyikia, kilifanyika wakati gani na pia kilifanyika mara ngapi. Kutokana na hayo tunapata aina nne za vielezi ambazo ni; Vielezi vya Namna au jinsiVielezi vya MahaliVielezi vya Wakati naVielezi vya Idadi Aina hizi za vielezi zinaelezwa moja baada ya nyingine hapo chini. Vielezi ya Namna au Jinsi Hivi ni vielezi ambavyo hutoa taarifa kuhusu namna au jinsi kitendo kilivyofanyika. Kwa mfano, Juma anatembea taratibu.Musa huja kwa kujivuta vuta.Baba alisononeka sana.Gari moshi li...