Sunday, July 5Kiswahili kitukuzwe!

Day: August 6, 2019

Sarufi

Vivumishi vya Kiswahili Sanifu

Kisemantiki, kivumishi ni aina ya neno ambalo hueleza zaidi kuhusu nomino au kiwakilishi. Kwa kuwa kivumishi hueleza zaidi kuhusu aina hizo za maneno. Hivyo basi, vivumishi haviwezi kusimama katika sentensi pasina nomino au kiwakilishi. Kimofolojia, kivumishi ni aina ya neno ambalo hujengwa na kiambishi cha upatanishi pamoja na mzizi wa kivumishi. Kwa mfano. m - zuri, ki - zuri, ki - bovu n.k. Aina za Vivumishi Vivumishi huweza kuwekwa katika aina mbalimbali kama ifuatavyo: Vivumishi SifaVivumishi IdadiVivumishi VioneshiVivumishi Viulizi (vya Kuuliza)Vivumishi VimilikishiKivumishi Kirejeshi (Vivumishi Rejeshi) Vivumishi Sifa Hivi ni vivumishi viaevyoelezea zaidi kuhusu sifa ya nomino au kiwakilishi. Tazama mifano hapo chini inayoonesha aina ya vivumishi hivi: Mtoto...